Pages

Saturday, August 22, 2015

MANCHESTER UNITED YABANWA KOO NA NEWCASTLE

Schweinsteiger akigombea mpira na kiungo wa Newcastle United

Matumaini ya kuendeleza wimbi la ushindi wa asilimia 100 kwa Manchester United yaliingia doa baada ya kushikwa shati katika mechi ilioisha kwa droo ya bila mabao pale Old Trafford.
Kipa Mholanzi Tim Krul alifanya kazi yan ziada kuokoa michomo ya Juan Mata katika kipindi cha kwanza kabla ya kumkatalia Hernandez Chicharito kipindi cha pili.

Bastian Schweinsteiger alianza kwa mara ya kwanza kabla ya kumpisha Michael Carrick katika duru ya pili ya mchezo ambao United walitawala kwa asilimia kubwa. United ambayo inamtumia Rooney kama mshambuliaji wao imefanya mashambulizi mengi kupitia kwa Rooney na Depay huku wageni nusura wapate bao dakika ya 24v baada ya Mitrovich kupiga mpira uluiogonga mwamba wa lango la United.
Rooney sasa amecheza mechi 10 bila ya kufunga goli na wiki iliopita aliwatoa wasiwasi mashabiki wa United baada ya kuahidi kuwa magoli yatakuja. United inahaha kupata mshambuliaji baada ya Rooney kuonekana kupwaya sehemu hiyo huku zikiwa zimebaki siku 10 tu kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Wiki iliopita Van Gaal alisema anaridhishwa na safu yake ya ushambuliaji lakini inahitajika afanye maamuzi ya haraka kabla dirisha la usajili kufungwa.

No comments:

Post a Comment