Pages

Friday, August 7, 2015

MCHAKA MCHAKA WA URAIS MAREKANI WAANZA KWA KASI

Tukiwa katika harakati za kueleka katika uchaguzi mkuu wa Tanzania October 25 mwaka huu, nchini Marekani Chama cha Republican kimeanza mchakato wa kuchagua mgombea mmoja atakae peperusha bendera ya Chama hicho katika uchaguzi mkuu utakao fanyika Agust 2016.
Wagombea urais wa Republican kutoka kushoto, Chris Christie, Marco Rubio, Ben Carson, Scott Walker, Donald Trump, Jeb Bush, Mike Huckabee, Ted Cruz, Rand Paul, na John Kasich.

Katika mdahalo uliofanyika nakurushwa na kituo cha Fox Nchini marekani ambapo Bilionea Donlad Trump  akionekana kupewa nafasi kubwa kwakile kinachoelezwa msimamo wake katika sera za uhamiaji na uchumi.

Kinya nyang'anyilo cha mwaka huu kina mvuto wakipekee ikizingatiwa kuna Bilionea machachari Donald Trump, kaka wa George Walter Bush na Daktari mweusi Ben Carson je? Marekani itampa mtu mweusi tena nafasi ya kuongoza? au kuweka mtu wa koo ya Bush katika White House? ni maswali machache yatakayo leta changamoto ndani ya uchaguzi huu ndani ya chama cha Republican.

Kwa upande mwingine Mama Hillary Clinton anaendelea na kampeni zake kupia chama cha Demokratic ambapo mpaka sasa ni mwanamke pekee aliejitokeza kuomba kuteuliwa na Chama cha Demokratic kupeperusha bendera ya chama hicho.
Hillary Rodham Clinton

POST POWERED BY: UGABWA SHOP

No comments:

Post a Comment