Kocha wa klabu ya Chelsea Mreno Jose Mourinho amesaini mkataba mpya utakaomuweka Stamford Bridge hadi mwaka 2019. Mourinho ambae amewshinda mataji matatu ya ligi kuu Uningereza akiwa na Chelsea amesaini mkataba wa miaka minne mbele ya msimu mpya wa ligi kuu ya Barclays utakaoanza kesho mchana.
Ripoti zinasema kuwa Mourinho, 52 alikua tayari kusaini mkataba mpya baada ya kufurahia msimu uliopita kwa kutwaa ubingwa wa England na Kikombe cha Ligi akiwa na kikosi hicho. Mourinho alirudi Chelsea baada ya kuzifundisha kwa mafanikio klabu za Inter Milan ya Italia na Real Madrid ya Hispania.
Chelsea itaanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kesho itakapoivaa Swansea City katika dimba la Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment