Pages

Friday, August 7, 2015

MANCHESTER UNITED YAFIKIA MAELEWANO BEI YA PEDRO NA BARCELONA



Manchester United and Barcelona wamefikia maelewano juu ya bei ya Pedro, ingawa mabingwa hao wa Hispania hawatopenda kumuachia hadi mechi ya UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla ipite jumanne ijayo.

Pande hizo mbili zimeelewana bei kuwa ni pauni18.1 million (€26m) kukiwa na vipengele vya bonus hadi pauni 4.2m (€6m).
Barcelona wanashindwa kumuachia Pedro hadi mechi ya Super Cup ipite kwa sababu mchezaji wao tegemeo Leonel Messi hayuko kwenye hali nzuri kucheza mechi hiyo akiwa ametoka mapumzikoni majuzi baada ya kupewa likizo fupi baada ya michuano ya Copa America. Mechi ya Super Cup itawakutanisha Barcelona na Sevilla katika mji wa Tbilisi jumanne ijayo na Barcelona wanaona kuna umuhimu wa kuwa na Pedro kwa sababu Neymar na Messi wana hatihati ya kucheza kikamilifu.
hiyo ina maana kuwa Manchester United ikifanikiwa kumsaimnisha Pedro hapo baadae italazimika kucheza mechi yake ya kwanza ya ufunguzi wa Ligi Kuu Uingereza bila ya huduma ya winga huyo wa Kihispaniola.

No comments:

Post a Comment