Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha ADC, Chief Yemba amemkaribisha aliekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF Prof Ibrahim Lipumba katika chama chao ikiwa atafanya maamuzi ya kutafuta chama kingine. Chief aliyasema hayo leo majira ya saa 5 asubuhi katika ofisi za NEC alipotoka kuchukua fomu za kugombea urais wa Oktoba mwaka huu .
Chief alisema CUF imejaa ukiritimba na udhalimu jambo linalopelekea viongozi wengi kukimbilia vyama vingine. "Lipumba amekuwa mvumilivu sana na nampongeza kwa hilo kwa maana alitegemea mabadiliko lakini haikua hivyo hatimaye aametoka" aliongeza Chief. Ikumbukwe kuwa jana usiku katika kikao cha kuwatambulisha wagombea wa chama chao Chief Yemba alisema iwapo Prof Lipumba angejiunga na ADC kabla ya saa tano leo basi aangemuachia nafasi ya kushiriki urais Oktoba mwaka huu.
Naye mgombea mwenza, Hamad Abdulla alisema Prof Lipumba amefanya jambo la busara sana ila amesikitishwa na kitendo chake cha kukaa kando na siasa ilhali mchango wake bado ni muhimu sana. "Nani asiejua umuhimu wa Profesa Lipumba katika nchi hii, tunamuomba aje tuendeleze gurudumu la kisiasa ili tuweze kujenga Tanzania yenye maadili" alisema Abdulla.
Prof Lipumba alitangaza kuachia madaraka ya chama cha CUF jana mchana kitendo kilichozua mitazamo tofauti kwa wanazuoni wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment