Manchester United inaainika kuwa ni klabu kubwa duniani linapokuja suala la mchezo wa mpira wa miguu. Dhana hii imeendelea kuishi kwa mashabiki wengi wa mpira lakini kwa upande wa pili wa shilingi ambao unahusisha wachezaji wakubwa, hii kwao ni tofauti kidogo.
Tangu Sir Alex Ferguson aichukue Man United mwaka 1986 amefanikiwa kuijenga kuwa timu yenye mafanikio makubwa sana ndani na hata nje ya Uingereza. Dunia imeshuhudia vikombe vikubwa vikienda Old Trafford lakini sio vikombe pekee bali hata wachezaji wenye majina makubwa kutua Kaskazini mwa England kwa sababu ya mvuto uliojengeka ndani ya klabu hiyo. Ferguson akisaidiana na David Gill waliwezesha ujio wa wachezaji muhimu pale Old Trafford kama Dmitar Berbatov, Diego Forlan, Louis Saha, Cristiano Ronaldo, Robin van Persie, Wayne Rooney na Ruud van Nistelrooy. Kipindi hiki United ilikua na mvuto ambao uliwavutia wachezaji hasa linapokuja suala la kuhusishwa kusainiwa na United. Deal zilifanyika kwa uhakika na mwisho wa mazungumzo United walimpata mchezaji waliekua wanamhitaji.
Tangu Ferguson na David Gill waondoke United, hali imeanza kuwa tete kwenye upande wa usajili baada ya shughuli kuachwa kwa Ed Woodward. Manchester United imepoteza uhakika wa kupata mchezaji yeyote wanaemhitaji. Hali hii imethibitishwa katika kipindi cha misimu ya 2013-14-15 ambapo United imeshuhudia wachezaji ambao wanaaminika walikua na nafasi kubwa ya kutua Old Trafford kuishia upande mwingine.
David Moyes alikua mbioni kumsajili kiungo wa Barcelona Thiago Alcantara lakini mwishoni aliishia Bayern Munich. Moyes hakuchoka akahamia kwa beki wa kiingereza Leighton Baines lakini walishindwa kukamilisha dili hilo na Baines akabaki Everton.
Baines |
Kroos |
Wiki chache baadae huku mashabiki wa United wakisubiria Pedro atue Trafford, Chelsea wanafanikiwa kuwapokonya tonge mdomoni baada ya Woodward kujitoa kwenye mazungumzo na Barcelona juu ya mchezaji. Pedro anaishia Stamford Bridge huku Van Gaal akijawa na jazba kwa sababu alikiri kumpenda Pedro kama mbadala wa Angel di Maria alietimkia PSG baada ya kuwa na maisha magumu katika kikosi cha Van Gaal.
Wachezaji wengine waliowahi kuhusishwa kwa ukaribu wa kutua Old Traford ni pamoja na Nikolas Otamendi ambae jana amesaini mkataba wa miaka mitano na mahsimu wakubwa wa United, Manchester City, Sergio Ramos, Matt Hummels, Cesc Fabregas na Gareth Bale ambao uendeshaji wa sajili zao uliendeshwa kizembe na Woodward.
Ramos |
Kuna kazi kubwa ambayo United inabidi kufanya kurudisha mvuto kitu kitakacholeta wachezaji wakubwa ambao wanawahitaji sana sokoni na lawama zinamrudia Woodward. Kipindi hiki United inahitaji mshambuliaji kutokana na kuondoka kwa Robin van Persie huku Wayne Rooney akihaha kuifanyia haki nafasi hiyo. Kuna kazi ya ziada ya kufanya kwa Woodward na United yote kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment