Monday, August 31, 2015
MANCHESTER MAZUNGUMZONI NA KINDA WA MONACO
Kinda Anthony Martial ameruhusiwa na Chama cha Soka cha Ufaransa kuacha kambi na kupanda ndege hadi Manchester kwa ajili ya kukamilisha dili litakaloigharimu United milioni 60 Euro.
United inahah kupata mshambuliaji baada ya safu ya ushambuliaji inayoongozwa na Wayne Rooney kushindwa kufanya chochote na kuambulia magoli mawili tu katika mechi tatu za Premier League.
Kumezuka wasiwasi mkubwa kuhusiana na usajili huu baada ya kutajwa bei hiyo hasa ukizingatia kinda huyo ndio kwanza ana miaka 21, swali ni je, ataweza kuthibitisha uthamani wake wakati amecheza msimu mmoja tu wa ligi ya wakubwa kwa AS Monaco?
Kinda huyo amefunga magoli 9 na kutengenza mengine matatu katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligue 1.
Labels:
Michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment