Pages

Wednesday, August 12, 2015

HILLARYCLINTON AKUBALI KUKABIDHI BARUA PEPE ZAKE



Hillary Clinton akifanya mahijiano na mtangazaji wa CNN Christiane Amanpour


WASHINGTON

Aliekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani HILLARY CLINTON amekubali kuwasilisha mfumo mzima wa barua pepe yaake kipindi akiwa madarakani  kwa shirika la upepelezi la nchi hiyo FBI.
CLINTON anapata wakati mgumu kuhusu maamuzi yake ya kutumia Barua pepe binafsi wakati yupo madarakani hasa kipindi hiki anapo tarajia kugombea uraisi kwa kupitia chama cha Democratic.
Pia wanasheria wa CLINTON watawasilisha maelfu ya nakala za barua pepe kwa FBI ikiwa ni katika kile kinachoelezwa ni kujisafisha kabla ya kampeni za kura za maoni dani ya chama hicho hazijaanza.
Matumizi ya Barua pepe binafsi badala ya ofisi imekuwa gumzo katika harakati zake za kusaka uras kwa  maswali mbalimbali kuibuka na watu kujenga hofu kuhusu uaminifu wake kwa serikali.

No comments:

Post a Comment