Dar es
Salaam.
Shirikisho la Michezo (SHIMIWI) linatarajia kuzindua mashindano ya
michezo yatakayoshirikisha watumishi wa Serikali kutoka katika Wizara, Idara
zinazojitegemea, wakala wa Serikali na Ofisi za Wakuu wa Mikoa
Akitoa taarifa hiyo
kwa waandishi wa habari Katibu Mkuu Kiongozi na Mkuu wa Utumishi wa Umma Balozi
Ombeni Sefue alisema mashindano hayo yatafanyika mjini Morogoro kuanzia tarehe
15 hadi 29 Agosti, 2015. Mpaka sasa vilabu
ambavyo vimejitokeza kushiriki mashindano hayo ni 47 tu.
Mashindano hayo
yatahusisha vilabu kutoka wizarani ambavyo ni; Ikulu, Utumishi, Waziri Mkuu,
Afya, Ardhi na Makazi, Elimu na mafunzo ya Ufundi, Hazina, Kilimo na Chakula.
Vilabu vingine ambavyo vitashiriki ni kutoka Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maji,
Wizara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Mambo ya
nje, Wizara ya Mambo ya ndani, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa,
Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Viwanda na
Biashara, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, na Tume ya Mipango.
Makuka ameongeza
kuwa vilabu vingine ambavyo vitashiriki katika mashindano hayo ni kutoka katika
idara mbalkimbali ambavyo ni Idara ya Mahakama, Idara ya Utumishi wa Umma,
Ofisi ya Bunge, Tume ya kurekebisha Sheria, Tume ya Mahakama, Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi ( NAO), na Tume ya Ushirika.
Vilabu vingine
ambavyo vimejiunga kushiriki Mashindano hayo ni vilabu kutoka katika wakala
mbalimbali ambavyo ni Wakala wa Jiolojia Tanzania, (GST), Wakala wa Ukaguzi wa
Madini (TAA), na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA),
Pia alisema
kutakuwa na vilabu kutoka katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa ambavyo ni; Lindi,
Katavi, Mwanza, Kagera, Rukwa Dar es Salaam, Mtwara, Iringa, Geita, Kigoma,
Manyara, Mara, Arusha na Tanga.
Vilabu ambavyo
vitafungua mashindanoi hayo ni Wizara ya Elimu dhidi ya Hadhina (Mpira wa
miguu), Wizara ya Afya dhidi ya Wizara ya Mambo ya nfdani(Mpira wa mikono), GTS
dhidi ya Wizara ya Mambo ya nje (kuvuta kamba kwa Wanaume), na Ikulu dhidi ya Bunge
(kuvuta kamba kwa wanawake. Mashindano hayo yote yataanza muda mmoja ambao ni
saa 4:00 Asubuhi.
No comments:
Post a Comment