Pages

Sunday, August 16, 2015

CHELSEA YAADHIBIWA VIKALI NA MAN CITY


Aguero akishangilia goli dhidi ya Chelsea
Sergio Aguero aliwekwa katika First Eleven ya Manuel Pellegrini baada ya kukosa mechi ya awali dhidi ya West Brom, huku Asmir Begovic akilinda lango la Chelsea baada ya Courtois kuwa nje kwa adhabu ya kadi nyekundu alioipata vs Swansea wiki iliopita. Haikuchukua muda kwa Aguero kupata goli la ufunguzi baada ya kupoteza nafasi nyingi za wazi kabla ya dakika ya 31. Man City walitawala mchezo mbele ya mashabiki waliojaa uwanjani Etihad, jijini Manchester.
Aguero akipongezwa na Raheeem Sterling na Kolarov baada ya kufunga goli la kwanza vs Chelsea

Kompany aliongeza bao la pili dakika ya 79 kabla ya Fernandinho kushindilia msumari wa maumivu kwa vijana wa Mouirnho dakika 6 baadae. Mourinho alimbadilisha John Terry kwa mara ya kwanza toka awe meneja wa timu hiyo akimuingiza Kurt Zouma katika kipindi cha pili lakini hali haikubadilika. Mbrazili Ramires aliipatia Chelsea bao la kusawazisha lakini sherehe yake haikufanikiwa baada ya mmoja ya wa maofisa wa mechi kunyanyua kibendera juu kuwa aliibia.
Diego Costa akizuiwa na Ivanovic (kushoto) na Fabregas baada ya kuzuka tafrani kati yake na Fernandinho wa City (hayupo pichani)

Eden Hazard alipata nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 70 lakini alipiga mpira kuymlenga Joee Hart huku Diego Costa akigonga mwamba kipindi cha dakika za nyongeza jambo ambalo hata kama angefunga lisingeharibu sherehe ya City. Kwa ushindi huo Man City wanaomgoza ligi wakiwa na pointi 6 pamoja na Leicester City na Manchester United wakitofoutiana tu magoli ya kufunga na kufungwa.
MATOKEO YA MECHI ZINGINE ZA EPL LEO NI KAMA IFUATAVYO
MCI
3 - 0
CHE
CRY
1 - 2
ARS
SUN
1 - 3
NOR
SWA
2 - 0
NEW
TOT
2 - 2
STO
WAT
0 - 0
WBA
WHU
1 - 2
LEI
SOT
0 - 3
EVE

No comments:

Post a Comment