Pages

Thursday, August 20, 2015

PEDRO HUYOOOOOO DARAJANI

Pedro

Chelsea iko katika hatua za mwisho kumsajili wimga wa Barceloma ambae amekua ni target ya muda mrefu ya Van Gaal. Jana jioni Manchester United kupitia katibu wake mkuu Ed Woodward walijitoa rasmi kwenye mazungumzo ya kumsajili Pedro anaetafuta muda wa kucheza baada ya kukosa akiwa Camp Nou kufuatia uwasili wa Suarez na Neymar.
Pedro alisafiri hadi London jumatano hii ili kufanya mazungumzo ya usajili huo. Van Gaal alikua anahaha kumsaini Pedro ili azibe nafasi ya Angel di Maria alietimkia PSG huko Ufaransa. Chelsea wamekubali kulipa dau la mil 30 ili kupata huduma ya winga huyo mshindi wa kombe la dunia 2010 na Euro Uefa 2008 na 12.

No comments:

Post a Comment