Pages

Tuesday, July 14, 2015

KONA YA SHERIA

Kuna mambo kadhaa unatakiwa kujua kama Raia, na kumbuka kutojua sheria hakuzuii wewe kuadhibiwa kwa kufunja Sheria hizo, basi hapa leo nimeamua kuwea baadhi ya mambo muhimu unayotakiwa kuyajua endapo utakamatwa na polisi au watakuja kwako kukuchukua kwa ajili ya mahojiano.

Pia ni muhimu sana kuwa na Mwanasheria Binafsi kwa aili ya kukushauri endapo utakuwa na tatizo la kisheria hapo ulipo, jitahidi sana kujua sheria za msingi maana zitakusaidia sana katika ufanisi wako wa kazi za kila siku.

Mambo hayo muhimu ni pamoja na;


  • Iwapo askari polisi ataamua kumpekua mtuhumiwa, mtuhumiwa ana haki ya kumpekua askari polisi KABLA ya kupekuliwa yeye mwenyewe
  • Pia, askari polisi hawana haki ya kuingia kwenye gari, nyumba au ofisi ya mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni ya kufanya upekuzi, pasi na kuwapo kwa (a) hati ya upekuzi ambayo hutolewa mahakamani, (b) mashahidi wanaotambulika rasmi kisheria, kama vile, mwenyekiti/mjumbe wa serikali ya mtaa au mwenyekiti wa nyumba kumi kumi (iwapo mfumo huo unatumika), au (c) jirani wa myu anayetuhumiwa
  • Aidha, mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na askari polisi baada ya saa 12.30 jioni au kabla ya saa 12.30 alfajiri, kwa mujibu wa Mwendendo wa Makosa ya Jinai (Penal Code Act), isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba, kumpekua mtuhumiwa kabla ya saa 12.30 alfajiri au baada ya saa 12.30 jioni kunaweza kuleta madhara kwa askari polisi, mashahidi au watu wengine wowote wale
POST HII KWA MSAADA WA JAMII FORUMS 
  •  
  •  
  • Raia ana haki ya kumwomba askari ajitambulishe kwako.
    • Mwulize jina lake
    • Mwulize namba yake ya uaskari
  • Raia ana haki ya kujulishwa kwanini anatiliwa mashaka ama kukamatwa.
  • Raia ana haki ya kuwajulisha ndugu, jamaa ama sehemu anakofanyia kazi kwamba ama amekamatwa na polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia ana haki ya kuomba na kupewa dhamana wakati akiwa kituo cha polisi ama Taasisi ya kuzuia rushwa.
    • Hutakiwi kutoa fedha kama dhamana uwapo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa, isipokuwa maelezo utakayoandika.
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
  • Raia ana haki ya kuomba Wakili wake awepo kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa wakati anatoa maelezo yake.
  • Raia ana haki ya kuyasoma kabla ya kutia sahihi yake.
  • Raia ana haki ya kudai risiti ya orodha ya vitu vyake/fedha zake alizozitoa ama kukabidhi kituo cha polisi ama Taasisi ya Kuzuia Rushwa.
  • Raia kama ni mwanamke ana haki ya kupekuliwa na polisi wa kike, na iwapo hakuna polisi mwanamke, basi mwanamke yeyote na vile vile kwa mwanamume.
  • Raia ana haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa kituo cha polisi.
  •  

No comments:

Post a Comment