Wanafunzi
wapya wanaojiunga na kozi mbalimbali katika Ngazi ya cheti na Diploma katika Chuo Kikuu
cha Tumaini Dar es salaam, wameaswa kutumia muda wao vyema katika kipindi cha
masomo yao.
Dr, Loth akizungumza na baadhi ya wanafunzi |
Akizungumza
na wanafunzi hao wakati wa hafla ya kuwakaribisha Dr Gillard Loth ambae ni
Muhadhili wa Chuo kikuu cha tumaini katika masomo ya Uchumi na Rasilimali watu,
ametaja baadhi ya mambo ambayo yana changia kupoteza muda kwa wanafunzi kama
vile simu za mikononi, urafiki uliopitiliza na Foleni.
Baadhi ya wanfunzi wakiwa katika hafla ya kukaribishwa |
Pia
akinukuu Maneno matakatifu kutokwa kwenye Biblia Eph3:20 Loth amesema Mungu
ameweka mambo Mengi sana ndani yamwanadamu na hivyo kuna ulazima wa kumtegemea
Mungu katika masomo na maisha ili kufikia malengo walio yaweka
Loth
amesisitiza kuwa muda wa kuwapo chuoni ni mchache sana na hivyo ni vyema
kutumia muda huo waliopata katika kujisomea ilikutimiza malengo yao. Pia
amesisitiza katika nidhamu baina ya wanafunzi na wanafunzi pia kwa wafanya kaziwa
Chuo.
Katika
kuhakikisha kuwa wanafunzi wapya wanajua wanayotakiwa kufanya Loth
amewakumbusha kusoma kwa bidii wawapo darasani, kujisomea vitabu ili kupanua
uwezo wa kufikiri akitolea mfano wa vitabu vya Think Big na Gifted Hands cha
mwandishi Ben carson na zaidi wametakiwa kuhudhuria vipindi vya darasani.
Dean of Students Mama Lema |
Pia moja ya mwanafunzi Francis Sylvester amesema amechagua kujiunga na Chuo cha Tumaini sababu ya Nidhamu inayopatikana Chuoni hapo na pia Elimu bora ambapo ametolea mfano wa kaka yake kuwa ni mmoja ya Tunda la Chuo kikuu cha tumaini Dar es salaam na anafanya vizuri katika soko la Ajira kama Mwanasheria.
Francis Sylvester |
MAINKAMPASI tunawatakia kila lakheri katika masomo yenu, penye nia pana njia!
TUNAWAKALIBISHA SANA CHUONI KWETU,,,,,,MAHITAJI MUHIM YANAYOTAKIWA KWA WANFUNZI YANAPATIKANA HAPA,,,,,
ReplyDeleteThnx Brother
DeleteTUNAWAKALIBISHA SANA CHUONI KWETU,,,,,,MAHITAJI MUHIM YANAYOTAKIWA KWA WANFUNZI YANAPATIKANA HAPA,,,,,
ReplyDeletekaribuni sana wapendwa all are possible
ReplyDeleteThnx Sister
Delete