jengo jipya la chuo kikuu cha Tumaini |
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini wameupongeza uongozi wa
chuo hicho kutokana na kuongeza jengo jipya ambalo linakidhi mahitaji yao ya
kila siku hasa kwa upande wa elimu.
Jengo hilo jipya lina ghorofa tisa ambapo ndani yake lina
madarasa (28), kuna maktaba na ofisi za kitivo cha sheria, kuna kanisa, ukumbi
mdogo wa mikutano na ukumbi mkubwa wa mikutano katika ghorofa ya tisa, katika
kila darasa kuna camera kwa ajii ya ulinzi na spika.
Mmoja wa wanafunzi hao ambae anayefahamika kwa jina la Mary Siame anayesomea shahada ya UALIMU mwaka wa pili amesema
najisikia fahari sana kuwa miongoni mwa wanafunzi wanaofaidika na elimu
inayopatikana hapa chuoni na nilikua na ndoto .
Ameongeza kua jengo jipya kwa sasa linachukua wanafunzi wengi
wakiwemo wa cheti (certificates) stashahada(diploma) na shahada(degree).
mmoja wapo wa wajumbe akichangia mada katika ukumbi wa mikutano na midahalo |
No comments:
Post a Comment