Karibu sana katika kipengele maalumu
kilichoandaliwa na Mwanafunzi Muyonga Jumanne (JAY 4). Dhumuni ya hiki kipengele ni
kupata taarifa katika maswali matano (5) kuhusiana na mada tofauti kama
taaluma, burudani na jamii inayomzunguka katika Chuo Kikuu cha Tumaini Dar Es
Salaam.
1. UNAITWA NANI?
"Naitwa EVELYN GASPER, nipo mwaka wa pili
kitivo cha mawasiliano kwa umma (mass communication). Napatikana Instagram GEVELIYM
au Facebook -
EVE GASPER".
2.UNAIZUNGUMZIAJE TUDARCO?
"Ni moja ya Chuo
kizuri katika vyuo bora Tanzania, kimenipa kujua mengi ambayo sikuweza jua
kipindi cha nyuma. Nimejua mengi katika masomo na mazingirayanayonizunguka hapa
Chuoni".
3.USHAURI JUU YA TUDARCO?
"Nina mambo
mawili ya kushauri katika kuboresha Chuo changu cha Tumaini, la kwanza ni upatikanaji
wa namba za mtihani, naweza sema zinashusha ufaulu wa wanafunzi kwakuwa wengi
wanakosa muda wa kujiandaa vizuri kimawazo kwa kuwaza jinsi ya kupata namba.
Chuo kiweke utaratibu mzuri wa upatikanaji namba kwa mtu alielipa mapema. La
pili ni ufinyu wa upatikanaji wa vitabu vya kukidhi mahitaji ya wanafunzi
katika maktaba, ningeshauri Chuo kipate vitabu vya kutosha".
4.
UNAJIVUNIA AU HUJIVUNII KUWA MWANAFUNZI WA TUMAINI?
KWANINI?
"Ndio najivunia,
kwanza najivunia kwa kupata nafasi ya kuchaguliwa hapa si wote waliotamani
kusoma hapa wamepata nafasi hiyo. Pili ni maarifa ambayo nimeyapata hapa Chuoni
yameweza kunisaidia mpaka sasa naweza kusimama mtaani na kuonekana msomi huku
uwezo wa kufanya jambo kama msomi umeongezeka pia zaidi. Nitajivunia miaka yote
kuwa mmoja wa wanafunzi wa Tumaini, Dar es Salaam".
5. KWANINI MAWASILIANO KWA UMMA (MASS COMMUNICATION) NA
SIO KOZI NYINGINE?
"Nimechagua kusoma Mawasiliano kwa Umma
kwanza ni kozi yenye wigo mkubwa katika usomaji, tofauti na watu wanavyozani
kuwa ni uhandishi wa habari. Pia nitakuwa mwakilishi wa sauti kwa wale
wasiosikika na wale wenye kuonewa".
Thanks broo
ReplyDelete