PICHA INAYOONESHA BAADHI YA WAJANE. |
Ikumbukwe kuwa siku hiyo ilibuniwa mwaka 2005 na LORD RAJ LOOMBA baada ya kumpoteza baba yake mzazi mwaka 1997,ikiwa ni njia moja wapo ya kumkumbuka mama yake aliyeachwa mjane akiwa na umri wa miaka 37 katika eneo la Punjab nchini India.
Licha ya siku hiyo kubuniwa mwaka huo,ilikuja kutambulika rasmi na shirika la umoja wa kimataifa(UN) mwaka 2010,na kuanza kuazimishwa katika mataifa tofauti yakiwemo Uingereza,Marekani,India,Kenya,Syria,Rwanda,Afrika ya kusini.Hatimaye mataifa mengine yakifuta kuiazimisha siku hiyo.
Madhumuni ya siku hii yamekuwa ni kuwatetea na kuwapatia elimu watoto yatima na wajane dunia kote,utafiti unaonyesha kufikia mwaka huu(2015) kuna zaidi ya wajane takribani millioni 245 duniani.Na wengi wao wanaishi katika mazingira magumu ikiwemo ukandamizwaji na unyanyasi uliokithiri.
Kwa upande wa Tanzania mwenyekiti wa chama cha wajane Tanzania(TAWIA) mama ROSE SARWELL bado anakabiliwa na kazi nzito ya kuwasaidia wajane,baada ya idadi kubwa ya wanawake kudai kulazimishwa kurithiwa na ndugu za mume pale inapotekea waume zao wanapopoteza maisha.Hivyo kuchochea ongezeko la ugonjwa wa Ukimwi.
WANACHAMA WA TAWIA. |
PICHA YA INAYOONESHA MAISHA HALISI YA MJANE. |
No comments:
Post a Comment