![]()  | 
| Mhasibu wa Tudarco, Yvonne Mmbando akisisitiza jambo ofisini kwake. | 
Wanafunzi
wametakiwa kulipa ada mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kuelekea
maandalizi ya mitihani yao.
Hayo yamezungumzwa
na  Mhasibu wa Chuo cha Tumaini Dar es
salaam YVONNE MMBANDO, wakati akitolea maelezo kuhusu upatikanaji wa namba za
mtihani ambazo zitaanza kutolewa kuanzia Jumatatu ya  Juni 26 mwaka huu, huku mitihani ikitarajiwa
kuanza July 6 mwaka huu.
Ada ya mwaka wa kwanza ni Tshs 2,405,000, mwaka wa pili Tshs 2,330,000 
na mwaka wa tatu Tshs 2,365,000. Pamoja na ada wanafunzi wote wanatakiwa
 wawe wamelipa hela ya TCU Tshs 20,000 na TUSO Tshs 25,000.

No comments:
Post a Comment