Kutokana na kukithiri kwa tatizo la ajira nchini,
vijana wengi wameamua kujishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali
ili kujipatia kipato na kuondokana na njia haramu ya kujipatia mali.
Mmoja wa wajasiriamali ambae anajulikana kwa jina la
Bariki Blastus anayejishughulisha na
upandaji wa aina mbalimbali za maua
katika eneo la pembeni ya Chuo Kikuu cha
Tumaini, amelezea faida kubwa
anayoipata katika shughuli yake ya upandaji na uuzaji wa maua.
Ameongeza kuwa, kutokanana kazi anayoifanya
anaingiza kiasi kikubwa cha fedha kwani kwa siku anaweza kuuza miche ishirini
hadi hamsini, na kila mche una bei yake kuanzia shilingi elfu mbili hadi elfu
kumi.
Ameeleza kuwa,
kutokana na kazi anayoifanya anaweza kujikimu na mahitaji yake yote ya
msingi kama vile chakula, malazi na mavazi na hata kutoa msaada kwa ndugu zake
pindi wanapokua na shida mbalimbali za kifedha.
Kutokana na faida kubwa anayoipata, amebainisha
changamoto kadhaa ambazo anakumbana nazo katika majukumu yake ya kila siku
ambayo ni pamoja na kutokuwepo kwa maji ya uhakika kwani mara nyingi yanakuwa
ni ya msimu, kukosekana kwa wateja kwani
mpaka maua yanakua makubwa na yanakomaa na kutofaa tena kwa kuuza, na pia hali
ya hewa pia ni changamoto, kwani sio maua yote ambayo
yanahimili hali ya hewa ya joto.
Hata hivyo, amewaasa vijana wengine kujitafutia
shughuli za kufanya ili kuweza kujipatia kipato chao halali na kuondokan na njia haramu
za upataji wa fedha kama vile uporaji na unyang’anyi.
mkulima wa maua akipalili bustani yake |
No comments:
Post a Comment