Pages

Tuesday, June 23, 2015

SIMBA YAMNYAKA MCHIZI WAKE MOURINHO



DYLAN KERR AKIWA MZIGONI.
 Timu ya soka ya Simba imefanikiwa kumpata mwalimu mkuu atakae kiongoza kikosi hicho,ikiwemo katika kampeni zake za kutaka kuwania kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya vodacom  inayotarajiwa kuanza mwezi september mwaka huu,DYLAN KERR, 48 raia kutoka uingereza ndiye anatarajiwa kuja nchini kuendeleza kuutafuna mfupa uliomshinda mkufunzi mwenzie kutoka Serbia KUPONOVIC.

KERR mwenye uzoefu wa takribani  zaidi ya miaka 30, anatambuliwa na shirikisho la kabumbu dunia FIFA kwa kuwa mwalimu mwenye leseni daraja ''A"aliyoipata mnamo mwaka 2001 akiwa na kocha mkuu wa Chelsea  JOSE MOURINHO,Kwa upande wa rekodi wakati akisakata soka aliweza kuzichezea timu mbalimbali zikiwemo Shefield Wesdney,Reading ,Blackpool pamoja na Leeds United zote za Uingereza.


KERR AKISISITIZA JAMBO.
Vile vile kocha huyo ameweza kuvifundisha vilabu mbalimbali kutoka Asia,Ulaya na Afrika ikiwemo Haiphong fc iliyopo ligi kuu ya Vietnam,ambapo alianzia kama kocha msaidizi wa timu hiyo kuanzia mwaka 2011-2013,mpaka alipopandishwa cheo mwaka 2014 na kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.

 Licha ya kufanikiwa kushinda kombe la ligi akiwa na timu yake,mkufunzi huyo anatarjiwa kupambana na changamoto mbalimbali katika ligi kuu ya vodacom punde tu atakapoingia nchini kukinoa kikosi hicho chenye makazi yake maeneo ya Msimbazi Kariakoo,Dar es salam.

No comments:

Post a Comment