Wiki nyingine yenye pilikapilika za maandalizi ya mitihani kwetu hapa tumaini na kwa wengine ni wiki ya kuanza mitihani yao ya kumaliza mwaka wa chuo yani UE
Kwa wenzetu wa IFM wanaanza mitihani yao jumatatu ya wiki hii na kutarajiwa kumaliza jumatatu ya tarehe 13 mwezi wa saba. Kuna kila sababu ya kuwapongeza kwakufika juma hili na tunawaombea kila la kheri katika mitihani yao ili waweze kufanya vyema.
Wanaomaliza mwaka kabisa yaani mwaka wa tatu tunawaombea Kheri na mafanikio katika maisha baada ya kumaliza mitihani yao.
Kwa niaba ya wana IFM George Kitindi na Mevis Mwampaja pokeeni salamu kutoka kwetu MAINKAMPASI
No comments:
Post a Comment