Mkuu wa chuo
cha Tumaini Dar es salaam (TUDARCO) profesa Uswege Minga ameshangazwa na idadi
kiduchu ya wanafunzi waliohudhuria katika kikao kilichofanyika leo kati yake na
wanafunzi.
Akifungua
kikao hicho mkuu huyo wa chuo cha TUDARCO ameshangazwa na hali ya wanachuo
kutokuhudhuria kikao hicho kutoka na
ukweli kwamba nafasi yake kukut ana na wanachuo kujadili maswala mbalimbali
chuoni hapo kuwa finyu na adimu.
Aidha baadhi
ya wanachuo walioshindwa kuhudhuria kikao hicho ambao majina yao pamoja na
vitivo vyao havikuweza kufahamika kwa haraka wameonyeshwa kukerwa na kitendo
cha serikali ya wanafunzi chuoni hapo (TUSODARCO) kwa kushindwa kupanga siku na
muda ambao idadi kubwa ya wanachuo wangeweza kuhudhuria.
Kutokana na
ukweli kwamba siku ya ijumaa katika muda
uliopangwa idadi kubwa wanachuo hawana
vipindi na kutokuwepo katika eneo la chuo.
Kikao hicho
kimefanyika siku ya leo katika majira ya saa 10 alasiri katika ukumbi wa
mikutano uliopo katika chuo hicho.Na kimekuwa cha kwanza kuwakutanisha wanachuo
pamoja na uongozi wa chuo cha TUDARCO baada ya kupita mihula(semisters)
takribani sita.
No comments:
Post a Comment