Pages

Saturday, August 15, 2015

BARCELONA YAANGUKIA PUA SUPER CUP

Kocha Mkuu wa Barcelona Luis Enrique
San Jose aliipatia Athletic Bilbao goli la kuongoza dakika ya 13 ya mchezo ambao Barca walitawala kwa sehemu kubwa. Kipindi cha pili kilianza kwa wageni kutafuta goli la kusawazisha lakini Aduriz Aritz alipoongeza goli la pili ambalo liliifanya Barcelona ipate wakati mgumu zaidi. Aduriz alioneekana kuwa na jioni njema zaidi kwa kushindilia msumari mwingine kwa kuongeza goli la nne hivyo kuzamisha kabisa matumaini ya mabingwa wa Hispania kunyakua Super Cup ambayo itarudiwa jumatatu pale Camp Nou.
Kocha wa Barcelona amesema anastahili lawama zote akiongweza kuwa kikosi kilikua na siku tatu tu za kujiandaa na mechi ya Super Cup baada ya kutoka nchini georgia ambako walikipiga na Seville katika UEFA Super Cup mechi iliowalazimu Barcelona kushinda katika kipindi cha nyongeza baada ya kuwa 4-4 katika dakika 90 za kawaida

Ukuta wa beki ya Barcelona unaonekana kuwa sio imara kwa sasa baada ya kuruhusu magoli manne katika mechi dhidi ya Seville baada ya Barca kuongoza kwa bao4-1. Andres Iniesta amesema ana matumaini kuwa watabadilisha matokeo katika mechi ya jumatatu
.

No comments:

Post a Comment