Imeandaliwa na Jay4
“Mjini mipango” ni moja ya kauli maarufu sana kwa watu watafutaji wa
maisha na wenye hasira ya maisha. Ndivyo ilivyo kwa watu wenye kufikiri mbali
ya pale walipo na kufikiri zaidi katika maarifa wapatayo yatakuwa na msaada
gani katika maisha ya baadae. Mwanamke mchapakazi, muangaikaji na mkombozi
kwa wanawake alipata nafasi ya kukutana na mwandishi katika maswali matano.
1.
Unaitwa nani?
“Naitwa
Jacqueline Dastan Shinado. Ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika kozi ya BBA
(Bachelor of Bussiness Administration). Napatikana Instagram kama (JACQUELINE
DASTAN, Fabrajay_10).
Tayari kwenda katika biashara. Picha na Jay4 |
2.
Unaridhika na huduma ya kiwango cha
elimu kinachotolewa na Chuo Kikuu Cha Tumaini?
“Ndio
naridhika, kwa kuwa mfumo wa hapo awali ulionikuza kuelewa darasani ndo sawa
niliokuta hapa chuoni. Walimu nawaelewa na wamekuwa msaada kwa wanafunzi popote
unapowahitaji. Hii imepelekea hata Chuo kuwa na jina kubwa na zuri mtaani na
kwenye soko la ajira kwa ujumla”.
3.
Nani ‘Role modal’ wako?
“Oooh!!
‘Role modal’ wangu ni mama yangu mzazi tu, Leah Mbunda.
Mama Leah Mbunda katika pozi. Picha na Jay4 |
4.
Kwanini Mama yako?
“Nina
mengi ya kumuelezea kiukweli, ila kwa upande wa taaluma ni mwanamke ambae yupo
tayari kufanya chochote kuhakikisha naenda shule na kupata elimu nzuri. Pia
maisha yake aliyoyapitia najiona napita zile njia yeye alizopitia mpaka kuwa
hapa. Najivunia sana kuwa mwanae”.
5.
Wewe ni nani baada ya miaka mitano?
“Kwanza
mimi ni mfanyabiashara mkubwaa, kuanzia hapa nilipo japo nasoma ila naendesha
biashara tofauti mfano kuuza suruali,
vipodozi na mikoba ya wanawake. Nafanya
kwa kusambaza bidhaa kwa kutumia gari langu au natembea nazo mwenyewe katika
begi. Nasomea utawala wa Biashara na
miaka mitano mbele kikubwa nitachojivunia ni kuwa nina akili kubwa ya kutotegemea
ajira ila inategemea katika KUJIAJIRI
kutokana na mfumo wa ajira Tanzania, hivyo nitakuwa nimepata ujuzi mkubwa toka
darasani utakaoniwezesha kufikia ndoto zangu za kuwa mfanyabiashara kubwa
nchini na nje ya nchi. Ushauri kwa wanawake wenzangu ni kujituma ili tusiwekeze
akili na nguvu asilimia kubwa katika kuajiliwa ila tuongeze maarifa katika
sekta ya kujiajiri”.
No comments:
Post a Comment