Pages

Saturday, July 18, 2015

FIKIRI KABLA YA KUTENDA!

Wahenga walikua na misemo na kauli nyingi sana za kuhimiza uwajibikaji kama msemo usemao  fikiri kabla ya kutenda, kuuliza sio ujinga na misemo mingine, kama viongozi wanao tuongoza wange kuwa wanafata wahenga wasemavyo bila shaka makosa madogo madogo yasingelijitokeza.
Rais na Makamu wake wakiwa na baadhi ya mawaziri

Kuna mambo mengi sana yakujiuliza kwanini Serikali ya wanafunzi imehairisha Bash iliyopangwa kufanyika jumamosi hii pale azura beach Kawe, Binafsi wakati naambiwa kuna Bash nilifurahi sababu tuliahidi katika kampeni zetu kipindi nashirikiana na Khalifa Said katika kusaka kiti cha Urais.

Mungu ni mwaminifu, Khalifa akaukwaa Urais kwa tofauti ya kura 160 kwa maaana kuwa hoja zake zilikua zina uzito kiasi kwamba akamwacha mwenzake kwa umbali wa kura 160, nilitarajia kuona kwa uzito wa hoja zake angeweza kusimamia hadi Bash inafanyika, kwa bahati mbaya ama mkosi niite tukaambiwa hakuna bash tena badala yake tukapewa maneno matamu tamu  kwamba itafanyika nyingine baada ya kufungua chuo. 

Labda kwa wasio jua hili ni kwamba Maganga mwanafunzi wa  BAED mwaka wa tatu aliomba ifanyike Bash kabla ya wao kuondoka na Khalifa alikubali mbele yao nadhani hii ilikuwa danganyisha toto kwao maana imeshindikana wazi, japokuwa amejaribu lakini ameshindwa kwa hoja dhaifu.

Tuangalie sababu zilizo sababisha kuahirishwa kwa Bash, mosi serikali ya wanafunzi haina pesa sababu imekopesha wanafunzi walioshindwa kumaliza Ada, ni vyema kuwasaidia wenzetu na jambo la kupongezwa sana lakini kuanzia wanaandaa hii Bash hawakujua kuwa mfuko hauna pesa? Hawakuuliza kwa uongozi uliopita? kuna nini cha ajabu kilitakiwa kufanya kiasi kwamba pesa isitoshe? waweke wazi walikua wanataka bajeti ya shingapi ili kuwezesha Bash hii?

Pili wadhamini, yani kweli Baba unataka kupeleka watoto picnic alafu unataka Baba flani ndo agharamie kweli? this is too cheap! kwamba ndani ya 25000/ wanayotoa wanafunzi haitoshi mpaka udhamini tena? kuna haja tena ya kufikilia zaidi namna ya kuwafanya watu wa refresh bila ya wadhamini maana kwa mtindo huu kila siku mtaachwa kwenye mataa.

Natoa Rai kwa viongozi kufanya uchunguzi yakinifu kabla ya kufanya maamuzi ambayo yanakuja kuonyesha kuwa maamuzi yenu sio sahihi niyaku kurupuka ni bure kabisa kusaka ushauri kutoka kwa watu waliowahi kufanikisha haya mambo.

Narudia tena kusema kuuliza sio ujinga na fikili kabla ya kutenda. 

No comments:

Post a Comment