Mh. Kilenzi(kushoto) akiwa na Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Silaa |
Vijana wengi wametangaza nia ya kugombea nafasi mbalimbali
za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao wa mwezi Oktoba 2015, ambapo kutakuwa na
uchaguzi wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.
Kwa kutambua hilo, Bwana Hermani Kilenzi mwanafunzi wa
sheria mwaka wa tatu katika chuo cha Tumaini mwenye historia nzuri ya uongozi
hususani wa shule tokea shule ya msingi mpaka chuo kikuu, ametangaza nia rasmi
ili aweze kuteuliwa na Chama chake Cha Mapinduzi (C.C.M) apate ridhaa ya
kuchaguliwa na wananchi kuwa Diwani wa kata ya Kijitonyama.
“Nimeamua kuchukua hatua hii ili niweze kutatua matatizo ya
wananchi wangu wa kata ya kijitonyama hasa katika suala zima la usafi, ambapo
nitapanga siku maalumu ya kuungana na wananchi wangu tuwe tunafanya usafi
katika maeneo yote muhimu”. Hata hivyo
amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na wananchi ili waweze kutatua changamoto
za maji, kuziba kwa mitaro, na kuzibua chemba za vyoo.
Pia aliongeza kuwa atahakikisha atawatafuta wadhamini ili
waweze kuwasaidia vijana na wamama katika shughuli za ujasiriamali, kwani hayo
ni makundi ambayo hayana ajira ya uhakika.
No comments:
Post a Comment