Maji
ni uhai
Ni
jambo ambalo kila mtu analijua kutokana na umuhimu wake mkubwa katika maisha ya
kila siku ya mwanadamu yeyote ambaye kwa namna moja ama nyingine amejaliwa
kuvuta pumzi (ambaye anaishi.)
Maji
yanafaida nyingi sana kwa mwanadamu ikiwa ni katika matumizi yake ya kila siku
kama vile kunywa na kufanyia shughuli mbali mbali za nyumbani kwa mfano kupika,
kuosha vyombo na kufanya usafi wa hapa na pale. Matumizi ya maji hayaishii hapo
tu bali yapo mengine hata katika viwanda ambapo maji yanatumika kwa shughuli
mbali mbali kutokana na kiwanda husika
Bila
kwenda mbali sana, katika mwili wa mwanadamu maji yanachukua nafasi kubwa hii
ni pamoja na umuhimu wake katika utendaji kazi wake. Maji katika mwili yanachukua
hadi kufikia asilimia takriban 60 ambazo hutumika hasa katika kuupa mwili nguvu
kwa kupunguza kiasi cha joto mwili. kazi nyinginezo nyingi za maji ni katika
maswala ya kiafya ambapo hutumika kama dawa kwa baadhi ya magonjwa kwa
kuzingatia ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya waliobobea. Kumbuka hizo ni
kazi chache tu za maji na zipo nyingine nyingi.
Amini
husiamini, ingawaje maji yanaonekana kuutawala sana uso wa Dunia kwa asilimia
takribani 71 lakini yale yanayoweza kutumia na mwanadamu ikiwa na maana ya MAJI
SAFI NA SALAMA KWA KUNYWA yanachukua asilimia chache ambazo ni takriban 2.5 tu.
Hivyo
basi ni vyema kabla ya kutumia maji kwa kunywa kujua kwamba yanafaa kwa kwa
matumizi hayo kwa maana si maji yote uyaonayo baharini, ziwani, mtoni na
kwingineko yanapopatikana yanafaa kwa kunywa yakupasa kutambua ni asilimia
chache tu yafaayo kwa kunywa.
No comments:
Post a Comment