Pages

Thursday, July 23, 2015

BARAZA LA MAWAZIRI LIMEONGEZWA


Meshack King'ani (Naibu Waziri wa elimu)
Raisi wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Tumaini cha jijini Dar es Salaam, Rashid Khalifa Said amemteua Meshack Nazaleno King’ani kuwa naibu Waziri wa elimu, katika kikao kilichofanyika leo tarehe  23/07/2015 siku ya Alhamisi.

Kikao hicho kilijumuisha raisi wa serikali ya wanafunzi, makamu Raisi, waziri mkuu, Katibu mkuu pamoja na Mawaziri wote kutoka katika kila Wizara. kulikuwa na agenda kadhaa ambazo zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na kumtambulisha naibu Waziri wa elimu.

“Nimemteua Meshack Nazaleno King’ani kuwa naibu waziri wa elimu, ambapo atafanya kazi pamoja na waziri wa elimu, Jane Yohane. nimemuona kwa muda mrefu kuwa ni mchapakazi na ni hodari kwani amekua kiongozi wa darasa kwa muda wa mwaka sasa”  alisema raisi.

Kwa upande wake naibu waziri mteule amemshukuru Raisi kwa uteuzi alioufanya,  “namshukuru raisi kwa kuuona na kuutambua mchango wangu na mimi napenda nithibitishe kuwa sitamwangusha na nitatekeleza majukumu yangu kadiri ya sheria na taratibu za uongozi, kwani nimekuwa kiongozi wa darasa kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kuteuliwa kuwa naibu waziri wa elimu”  alisema meshack.

Jane Yohana(Waziri wa ELimu), Rashid Khalifa(Raisi) na Meshack King'ani (Naibu waziri wa elimu) kutoka kushoto.
Uteuzi huo unafanya kuwepo kwa mawaziri kumi (10) na manaibu waziri watatu (3) kutoka katika Wizara ya elimu, wizara ya fedha na Wizara ya michezo na burudani wakati wizara nyingine bado hazina manaibu waziri ni wizara ya utawala bora, wizara ya habari na mawasiliano, wizara ya sheria na katiba, wizara ya afya, wizara ya mambo ya ndani, wizara ya mambo ya nje na wizara ya mikopo.

1 comment:

  1. nawaaahidi ushiriano ili tufanikishe malengo yetu ,,,,

    ReplyDelete