Katika kuhakikisha kuwa Turdaco Speakers Bureau inafanikisha kuandaa Midahalo na matukio mengine ya kimaendeleo baadhi ya viongozi na wajumbe wa Bureau wametembelea ofisi za Soko la Hisa la Dar es Salaam Dar es Salaam Stock Exchange ili kujenga urafiki wa kimaendeleo.
|
Baadhi ya viongozi wa Bureau na Afisa miradi soko la Hisa Patrick Mususa(katikati) |
Moja ya mikakati ya Bureau ni kujenga urafiki wa karibu kati yake na mashirika mbalimbali ili kufanikisha mikakati iliyopangwa katika kalenda ya Turdaco'S Bureau, na Soko la Hisa la Dar es Salaam wameonyesha mwitiko wa kushirikiana na Bureau katika maandalizi ya Midahalo na matamasha.
|
Philip,Amidu,Ajrah,Patrick,Mahenge,Asela,Mapunda(kushoto) |
Katika mazungumzo yaliofanyika kati ya viongozi hao na Afisa miradi wa Soko la Hisa la Dar es salaam Patrick Mususa viongozi walipendekeza njia mahususi za kujenga urafiki kati ya Sokola Hisa na Turdaco'S Bureau moja ya mikakati ni pamoja na kuandaa Mdahalo utakaohusu Uchumi, Hisa na namna ya kukuza mitaji kwa kutumia soko la Hisa la Dar es Salaam.
Pia katika kuonyesha utayari wa Soko la Hisa katika kushirikiana na
Turdaco'S Speakers Bureau mara Chuo kitakapo funguliwa watashirikiana na
Bureau pale inapowezekana katika kuandaa mdahalo utakao lenga kuwa
elimisha wanafunzi juu ya shindano wanaloliendesha na linalolenga
kuwawezesha wanafunzi katika kufikiri vizuri katika kujenga mitaji kwa
kutumia soko la Hisa.
|
Kennedy Philip na Florid Mapunda wakisikiliza jambo kabla ya kuingia kwenye kikao |
Patrick Mususa alionyesha kukubaliana na mipango iliyopangwa na Bureau na kusisitiza katika kujenga urafiki kati ya Bureau na mashirika na Taasisi nyingine ili kuwa na wigo mkubwa wa kushirikiana katika maandalizi ya Midahalo na matamsha mengine yatakayo andaliwa na Turdaco'S Speakers Bureau.
|
Asela na Hajrah Bureau First Ladies |
No comments:
Post a Comment