Pages

Friday, June 26, 2015

OKOA MAISHA NA UJIOKOE KATIKA MAJI



Pamoja na uhuitaji mkubwa wa maji kwa ajili ya maisha, maji pia ni chanzo cha maisha kupotea. Baadhi ya mifano ya maisha kupotea  kwa maji ni pamoja na ajali za Meli, Mashua  na Mitumbwi lakini pia mafuriko na watu kutumbukia Visimani.
mkufunzi pamoja na wanafunzi mazoezini

Mkufunzi wa Uogeleaji ambaye pia ni Mkutubi (Librarian) wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Stewart Kiluswa anasema ni vizuri kujua hatari za maji na jinsi ya kujikinga nazo.

“watu wengi ufa maji kwa sababu hawajui hatari au jinsi ya kujiokoa au kuokoa wengine pindi wanapokuwa majini au maeneo ya maji, lakini kama mtu akijua hatua za kujikinga na kuokoa ni dhahiri maisha ya walio wengi hayatapotea kwa maji tena, chukulia mfano mafuriko ya juzi (mafuriko ya mwezi wanne mpaka wa tano) inasemekana watu karibia tisa wamepoteza maisha na inawezekana idadi ni kubwa zaidi, hii yote ni kwa sababu watu wahajui namna ya kujiokoa”.

Kiluswa anatoa wito kwa wanafunzi kujiunga na jumuiya ya Uokoaji maisha kwenye maji(Tudarco Life Saving)  ili wajue hatari za maji na jinsi ya kujiokoa, pia wapate kujifunza kuogelea.

boya la kuokolea


Katika hali ya kawaida unaweza kufikri kuwa wote wanaokufa maji hawajui kuogelea, lakini miongoni mwa wanaokufa maji wengine ni wataalamu wa kuogelea.  Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kupelekea watu kufa maji ikiwemo kutokujua hatari za maji au hatari zipatikazo majini.`
Hatari za maji ni pamoja na kutokujua hali ya maji, kutokujua sehemu hatari katika maji mfano sehemu yenye mkondo wa maji, kutokujua wanyama au wadudu wakali waliopo kwenye maji, pia kutokuwepo na alama za usalama maeneo ya maji.

Mwanafunzi akijifunza kuogelea
Moja ya hatua mathubuti za mtu kuchukua katika kuhakikisha kuwa yuko salama yeye na wanaomzunguka ni pamoja na kutambua hatari za maji, kujua namna bora ya kuokoa, kujua namna bora ya kujiokoa na kujua namna bora ya kumhudumia mtu aliyezama maji (huduma ya kwanza). Pia kuweka mazingira au vyombo ama visima vya maji vikiwa katika hali ya usalama muda wote.
Moja ya vitu ambavyo tunavitumia sana katika maisha yetu ya kila siku ni maji.  Wataalam wa sayansi wanasema kwa kiasi kikubwa mwili wa binadamu umechukua maji.

Ni vizuri tukajua matumizi sahihi ya maji na namna ya kuishi kwa usalama wakati wa matumizi ya maji.
Mwandishi wa habari hii ni mwana jumuiya ya Tudarco Life Saving, anapatikana kwa namba 0716539861

No comments:

Post a Comment