Pages

Saturday, June 27, 2015

MIAKA 12 YA KIFO CHA MARC VIVIEN FOE


Ilikuwa ni tarehe 26 ya mwezi june mwaka 2003 katika mchezo wa nusu fainaili katika mashindano ya mabingwa wa mabara baina ya Cameroon iliyokuwa ikipepetena vikali dhidi ya Colombia,Mchezo uliopigwa katika uwanja wa Stade Gerland uliopo katika jiji la Lyon nchini Ufaransa,Ghafla katika dakika ya 72  kiungo MARC VIVIEN FOE alinguka na kapoteza fahamu na baadae kutangazwa kuwa nyota huyo alikuwa amepoteza maisha wakati akiwahishwa hospitalini, tukio lililosababishwa na Moyo kusimama.

Marc Vivien Foe akitolewa uwanjani katika dakika ya 72 ya mchezo baada ya moyo kusimama
Tukio hilo lilipelekea simanzi katika jamii ya wapenda soka kote duniani,kutokana na kiwango kikubwa alichokuwa akikionyesha Kiungo huyo aliyekuwa akipendelea kuvaa jezi namba 17  katika timu yake ya taifa.

Jezi ya timu ya taifa ya cameroon aliyokuwa akiitumia Foe
Kipaji cha Foe  kilianza kuchomoza  mwaka 1994 pale alipojiunga na Canon Younde ambapo alifanikiwa kushinda kombe la ligi ya Cameroon, kiwango alichokionyesha msukuma kandanda huyo katika mwaka huo huo kilichochea kuitwa kufanya majaribio kunako klabu ya Auxere lakini kwa mshangao alisajiliwa na Lens  aliyoitumikia kwa muda wa  miaka mitano (1994-1999)Licha ya kutakiwa na Manchester United aliitupilia mbali ofa hiyo kiasi cha Euro kabla ya kutimkia Olympic Lyon (2000-2002) zote za ligi kuu ya ufaransa.Kipindi cha  mwisho wa uhai wake alisajiliwa kwa mkopo na kocha KELVIN KEEGAN wa Mancehester City (2002-2003) ambapo alionyesha kiwango murua kilichowakuna mashabiki wa soka hususani kwenye mchezo  dhidi ya Sunderland.


 
Foe kipindi akiicheza manchester city chini ya Kelvin Keegan
Baada ya kifo chake klabu yake ya zamani Olmpic Lyon alipokuwa akivalia jezi namba (17) pamoja na Manchester City jezi  namba (23) chini ya KEEGAN walitangaza kuzifungia jezi ziliyokuwa zikivaliwa na Kiungo huyo ikiwa ni  katika hali ya kuonyesha kuukubali uwezo  wake.Lakini baadae Lyon baada ya kumsajili mkameruni mwenzake JEAN II MAKOUN walimruhusu kutumia jezi hiyo ikiwa ni njia moja wapo ya kumuenzi marehemu FOE.


Maelfu ya watu waliohudhuria mazishi ya Foe.
Mpaka siku ya leo wapenda soka  wote dunia wanajumuika kwa pamoja kuadhimisha miaka 12 ya kifo cha nyota huyo,.ambaye stori yake imebakia midomoni na vichwani mwa wanafamilia wa mpira wa miguu hivyo kuendelea kukumbukwa na kusimuliwa kila mara..MARC VIVIEN FOE alizaliwa mnamo mei mosi ya mwaka 1975 katika jiji  la Yaounde,na maelfu ya watu walitiririka kuhudhuria mazishi yake yaliofanyika nchini Cameroon.




No comments:

Post a Comment