Pages

Tuesday, June 30, 2015

NEC YAPIGA KALENDA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAR NA PWANI.




Wakati zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura likiendelea vema kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.Tume ya uchaguzi kupitia kwa mkurugenzi wa uchaguzi  Bwana JULIUS.B.MALLABA ametangaza kuahirishwa kwa zoezi hilo katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

 
Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume Julius Mallaba akizungumza jambo.
Hatua hiyo imefuatiwa na  vifaa vya kielotroniki vya kujiandikishia wapiga kura(BVR) vilivyotarajiwa kutumika katika mikoa hiyo,kupelekwa kwenye maeneo ambayo yameripotiwa kuwa na idadi kubwa ya watu ambapo mchakato unaendelea mpaka hivi sasa.

Aidha taarifa zaidi kutoka mtandao wa tume hiyo zinadai kuwa vifaa hivyo vimelazimika kupelekwa katika mikoa mingine kutokana na ukweli kuwa mwamko miongoni mwa wananchi wanaojitokeza kujiandikisha katika daftari hilo kuongezeka.

Wananchi waliojitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Mchakato huo ulipangwa kufanyika kuanzia tarehe 25 ya mwezi June mwaka 2015 kwa mkoa wa  Pwani huku Dar es salaam ulitarajiwa kufanyika  tarehe 04 ya mwezi Julai mwaka huu.

Tume inawaomba wananchi wa mikoa iliyotajwa kuwa wapole, wakati wakisubiri tarehe husika kutajwa pamoja na vifaa hivyo kuwasili kutokea katika mikoa ambayo zoezi hilo litakuwa limekwikushamalizika.

MAINKAMPASI inatoa rai kwa wasomi wote kutoka TUDARCO na vyuo vingine kutokupoteza haki yao ya msingi ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. 

No comments:

Post a Comment