|
Gonzalo Jara akionyesha utovu wa nidhamu dhidi ya mchezaji mwezie Edinson Cavani |
Wakati duniani ikishangazwa na kitendo
cha ajabu na kisichokuwa cha kiungwana michezoni kilichotokea usiku wa jana
katika mchezo wa robo fainali ya mashindano ya kopa Amerika, kwa beki wa timu
ya Taifa ya Chile GONZALO JARA kumchoma
kidole mshambuliaji wa Uruguay na Paris
saint German(PSG) EDINSON CAVAN,Wadau
wengi wengi wa soka kote duniani wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na
tukio hilo. Licha ya adhabu
kali iliyotolewa na shirikisho la soka barani humo kwa kumfungia
mechi zote zilizosalia za mashindano hayo.
Kwa majina yake halisi anafahamika kama Gonzalo Alejandro Jara Reyes,alizaliwa
mnano mwaka 1985 tarehe 29 ya mwezi agosti katika mji wa Santiago nchini
Chile,alifanikiwa kuanza kuichezea timu ya taifa tokea mwaka 2006.Mpaka hivi
sasa anacheza soka la kulipwa nchini Ufaransa katika klabu ya Mainz 05.
|
Luis Suarez (9) akimtwanga ngumi Gonzalez Jara(18) |
Kunako mwaka 2004 katika mashindano hayo
mshambuliaji mwingine mtukutu toka
Uruguay LUIS SUAREZ alishutumiwa kwa
kumpiga ngumi JARA,tukio lililokuja
baada ya mlinzi huyo kuanza kurushiana maneno na baadae kutaka kujaribu
kumshika nyota huyo wa zamani wa klabu ya
Liverpool wakati akiwa katika purukushani za kutafuta bao.Pia anakumbukwa zaidi na mashabiki wa Chile kwa penalti yake
kugonga mwamba, katika mchezo wa robo fainali ya mashindano ya kopa Amerika
mwaka huohuo na kuipatia nafasi Brazil kufudhu katika hatua ya Nusu fainaili ya
mashindano hayo.
|
Penalti iliyopigwa na Jara ikigonga besela na kuitupa nje ya mashindano timu yake ya Uruguay |
Taarifa kutoka katika mtandao mmoja wa
nchini Hispania unaofahamika kwa jina la Latercera,zinadai tofauti na wachezaji
wengine wenye idadi kubwa ya wapenzi,Mlinzi huyo akiwa na umri wa miaka 19 aliweza
kumuoa mpenzi wake ROXANA,na
kufanikiwa kupata watoto wawili wa kiume
NICOLAS pamoja na LUCAS.
|
Jara akiwa na mkewe Roxana. |
Ikumbukwe mpaka GONZALO JARA anakumbwa na kashfa hii,amekwisha kuzichezea timu mbalimbali za kulipwa barani Ulaya zikiwemo West Bromwich Albino(2009-2013) pamoja na Northingham Forest(2013-14) za nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment