CV
 yenye  kujitosheleza ni njia muafaka ya kumfanya bosi wako mtarajiwa 
kukufahamu  wewe. CV nzuri inakupa nafasi ya kung’aa katika kikundi na 
kupata fursa  ya usahili na baadae kazi.
Pitia matangazo ya kazi
Unapopitia matangazo ya kazi katika magazeti, kuta za matangazo au barua
  pepe hakikisha unapitia matangazo hayo kwa umakini. Fanya maamuzi ya  
kipi kati ya ujuzi, sifa ama uzoefu utatumia katika kazi yako mpya.
Orodhesha vitu  
hivi na tumia maneno yenye kuonyesha vitendo kwa mfano : Mimi ni mtu  
mwenye mpangilio, ufanisi na mchapa kazi, nimeongoza na kusimamia watu  
na matukio.  Nimesoma na kufikia ubora katika weledi na kumaliza shahada
  ya kwanza katika…..
Kua sahihi kwa kutoa maelezo mafupi yenye kueleweka
Usizidishe maelezo kwa kutoa maelezo yote kukuhusu wewe, hakuna anayetegemea wala kutaka kuyasikia hayo kwa hiyo usifanye hivyo.
CV inatakiwa kumwelezea mtu lakini si kama kitabu kinachoelezea wasifu  
wako lakini pia si aya/ibara ama kitabu unachoelezea hadithi ya maisha  
yako ya weledi! Hakikisha huweki taarifa zako binafsi ambazo hazihusiani
  na nafasi unayoomba.
Sema ukweli
Kua mkweli. Kwa kufanya hivyo unaonyesha kujiamini na mafanikio yako na 
 hii itakusaidia inapokuja kukaa kwa ajili ya usahili. Huwezi kuzungumza
  kuhusu uzoefu wako kama mwanasayansi wa nyuklia kama hukufaulu masomo 
ya  sayansi shuleni!
Epuka makosa haya
Vitu vichache vya kuepuka kufanya: Usidanganye, usizidishe chumvi, usiweke ahadi usizoweza kuzitimiza.
Vidokezo katika kujielezea
Orodhesha majumuisho yako. 
Elezea CV yako katika lugha chanya. 
Inasaidia kama utaandika sentensi fupi na zenye kuonyesha uhai na kuepuka kutumia vivumishi vingi. 
Anza na mafanikio yako ambayo yanawiana na mahitaji muhimu ya kazi.  
Usimweleze mwajiri ni kwa vipi atakusaidia bali mueleze ni kwa vipi wewe
  utamsaidia. 
Tia msisitizo katika uzoefu unaohusiana na biashara ama kazi husika.  
Kama una uhusiano mzuri wa kazi na wataalamu katika fani yako unaweza  
kuwaomba kuwatumia kama wadhamini.
 Pata ushauri kabla hujatuma CV yako. Tafuta mtu unaemjua katika fani  
husika ili apitie CV yako. Jiandae kurekebisha vitu ulivyoandika.
Jaribisha CV yako kwa kuomba nafasi mbalimbali katika kiwango chako  
lakini pia kiwango cha juu kidogo. Hii itakusaidia kujua soko la ajira  
na thamani yako.
Isiwe sawa kila wakati
CV yako inabidi iwe inaendana na kazi unayoomba. Hivyo basi wakati  
unaomba kazi tofauti kwa kutumia CV ile ile ni vizuri ukajaribu kuiweka 
 CV ikaendana na nafasi unayoomba.
Usikate tamaa
Tumia CV yako kuitwa kwenye usahili. Huko utapata fursa ya kuelezea mafanikio yako. 
Kitu cha muhimu, USIKATE TAMAA! Kwa kila CV 100  unazotuma 
unaweza kuitwa kwenye usahili mara 10, na katika mara kumi  hizi utapata
 kazi moja tu- kazi yako ipo inakusubiria. Kua makini na  mwenye malengo
 na muda si mrefu utakua mmoja ya watu katika dunia ya  kazi.  Kwa ukina wa Habari hii tembelea bofya hapa  KUANDIKA CV                      Chanzo: http://www.mywage.org/tanzania-sw/nyumbani/kazi/kutafuta-kazi/andika-cv-nzuri                                                                                                     
Uko vizuri mkuu kwa kutoa hii elimu
ReplyDelete