Bwana Maganga akiwa anafanya kazi zake kwa umakini kuubwa |
Idadi wa Wanafunzi wa Chuo kikuu cha Tumaini
wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi wa ubunge na udiwani zinazidi
kuongezeka kadri ya siku zinavyozidi kwenda.
Mmoja wa wanaowania nafasi hizo ni Bwana Maganga Japheti Emmanuel ambaye ni
mwanafunzi wa Ualimu mwaka wa tatu, ametia nia rasmi ya kutaka kugombea ubunge
katika jimbo la Geita mjini kupitia
chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Akiongea na mwandishi wa
mainkampasi.blogspot alisema, “Nina kila sababu ya kutaka kugombea ubunge
katika jimbo la Geita ili niweze kuwaokoa wananchi wangu ambao ni maskini
wakati wana rasilimali za kutosha hasa mgodi wa madini wa Geita (Geita Gold Mine),
pamoja na uwepo wa hifadhi ya Taifa ya Rubondo
ambazo huingiza mapato makubwa.”
Hata hivyo alisema kuwa, mtu anayetaka
kugombea katika jimbo la Geita lazima azijue shida za watu wa Geita na namna ya
kuzitatua, lakini wabunge wote waliopita wameshindwa kuzitatua ili hali kuna
rasilimali za kutosha badala yake hujinufaisha wao wenyewe.
Bwana Maganga ameongeza kuwa CHADEMA ambayo ipo ndani (UKAWA), ndiyo chama pekee
ambacho kinajua matatizo ya wananchi na namna ya kuyatatua, na wananchi
wameteseka kwa miaka mingi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo huu ni mwaka wa ushindi na
mafanikio kwa wananchi kupitia CHADEMA.
Pamoja na hayo yote amesema kuwa amekuwa
ndani ya chama kwa miaka mingi na anajua mengi kuhusu chama chini ya uongozi shupavu wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, ambaye
ameweza kutatua matatizo mengi na kuleta mafanikio makubwa katika chama.
No comments:
Post a Comment