Solanus Elenziary Gumbo |
Akizungumza na mainikampasi amesema kuwa, ndani ya miaka miwili ya mwanzo atakuwa
ametimiza takribani asilimia 50 ya sera zake. Elimu yake ya Sekondari ameipata
Seminari, mara baada ya kuhitimu kidato
cha sita alijiunga na Seminari kuu kwa ajili ya elimu ya filosofia na
theologia, baadae akasoma shahada ya ualimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na
amesomea shahada ya udhamivu ya taaluma ya maendeleo katika chuo hichohicho.
Amejiunga na CHADEMA mwaka 2007, “Kilichonipelekea kujiunga
na CHADEMA ni kutokana na sera nzuri za chama na ziko kivitendo zaidi,
kulinganisha na vyama vingine, pia kuwepo kwa viongozi shupavu ndani ya chama
kama vile Halima Mdee, Tundu Lissu, Dr.
Wilbroad Slaa na wengineo wengi” aliongeza
bwana Gumbo.
Amesema kuwa, atahakikisha anasimamia suala la elimu kwa
shule zote za msingi na Sekondari, pia walimu wanapata nyumba nzuri na za
kudumu pamoja na upatikanaji wa vitabu vya kwa ajili ya shule zote katika jimbo
la Peramiho pamoja na, walimu wa kutosha na upatikanaji wa maabara na mabweni katika shule zote za Sekondari ili kuinua kiwango cha ufaulu
katika jimbo lake.
Gumbo akionesha ishara ya amani na upendo |
Pia ameahidi
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili waweze kuwasaidia wananchi
katika shughuli za ujasiriamali na, atahakikisha wananchi wa Jimbo lake
wanapata umeme, kwani wamehangaika kwa muda mrefu wakisubiri umeme tangu enzi
za uhuru (1961) mpaka sasa hawajaletewa,“hatuwezi kuwa na maendeleo bila ya
uwepo wa umeme ona nchi zote zilizoendelea kama Ujerumani, Chiina na Ufaransa
ni kutokana na uwepo wa umeme na hii inawezekana ndani ya nchi yetu”, alihoji
No comments:
Post a Comment