Pages

Thursday, September 3, 2015

DE GEA KURUDI MEZANI NA MANCHESTER UNITED

 De Gea considering Man Utd renewal after Real Madrid transfer collapse


Mlinda mlango wa klabu ya Manchester United, David de Gea atalazimika kurudi katika meza ya mazungumzo na bodi ya timu hiyo ili kuokoa nafasi yake katika timu ya taifa ya Spain.
De Gea ambae alikua karibu kujiunga na timu ya mji wake Real Madrid amebaki Old Traford kufuatia kucheleweshwa kwa taarifa za uhamishio wake jambo lililopelekea kulaumiana kati ya klabu hizo mbili.
Sasa de Gea atalazimuika kusainin mkataba mpya na mashetanmi wekundu ili aokoe nafasi yake ya ujumuishwaji katika timu ya traifa hasa wanapocheza mechi za kufuzu kombe la Ulaya mwakani nchini Ufaransa.
Wakala wa De Gea, Jorge Mendes amesema mteja wake yuko tayari kukaa mezani kwa ajili ya mazungumzo ya mkataba mpya.  Kocha wa Hispania Vicente del Bosque alimuonya de Gea kuwa kama anataka kujumuishwa kwenye maandalizi ya Euro 2016 basi apate muda wa kutosha katika ngazi ya klabu.
Kufeli kwa dili la kwenda Madrid kutamlazimu De Gea arudi mezani na United kwa ajili ya mkataba mpya ambapo awali United walimpa mkataba mnono lakini Mendez alisisistiza mteja wake anataka kwenda Real Madrid.
Kusainishwa kwa de Gea kutampa nafasi Keylor Navas ya kujiimarisha kama golikipa wa kwanza pale Bernabeu kama mrithi wa ngului Ikker Cassilas alietimkia FC Porto ya Ureno.

No comments:

Post a Comment