Mlinda mlango wa Manchester United David de Gea amerudi rasmi kwenye mazoezi ya timu hiyo baada ya uhamisho wake kwenda Real Madrid kufeli dakika za mwisho.
De Gea anarudi mazoezini huku Manchester United ikiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuwavaa mahasimu wao wakubwa Liverpool ma kuna uwezekano akaanza.
Mlinda mlango huyo aliwasili uwanja wa mazoezi jana na kuelekea moja kwa moja katika kipengele cha Maswali na Majibu kinachoandaliwa na wadhamini wa klabu hiyo ya magharibi mwa Uingereza.
Katika kipengele hicho de Gea aliongozana na kochja mkuu wa Mashetani wekundu Luis van Gaal huku kukiwa na uvumi wa wawili hao kukaa mezani hivi karibuni kwa ajili ya mazungum,zo ya mkataba mpya wa mlinda mlango huyo kutoka Hispania.
De Gea hajacheza mechi yoyote tangu kuanza kwa msimu huu huku van Gaal akimtetea kuwa hakuwa katika hali nzuri kisaikolojia kucheza kufuatia tetesi za usajili wake kwenda Madrid.
Kocha wa Hispania amemuonya DeGea kupata muda wa kutosha kwenye klabu ili aweze kwenda kwenye michuano ya Euro 2016 nchini Ufaransa juambo litakalomlazimu de Gea kusaini mkataba mpya ambao aliukataa hapo awali ili kujiumga na miamba hiyo ya Hispania.
MADRID KUTO,SAJILI DE GEA JANUARY
Rais wa Real Madrid amesema klabu yake haitajaribu kumsajili kipa huyo katika dirisha la usajili la january kufuatia kile alichokiita ni uzembe wa Man United katika kusimamia dili za dakika za mwisho kabla dirisha la usajili huku akikumbushia jinsi ilivyoshindikana kumtoa Fabio Coentrao kwenda United dakika za mwisho za dirirsha la 2014.
No comments:
Post a Comment