Pages

Wednesday, July 8, 2015

CHIMBUKO LA SIKUKUU YA SABASABA



Siku ya leo napenda nizungumzie maadhimisho ya siku ya sabasaba, nikuulize msomaji wangu unafahamu chimbuko la maadhimisho ya siku ya sabasaba?
Kwa upande wangu ilinipa wakati mgumu sana kuelewa lakini ukweli ni kwamba, ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 07/07/1954 ndipo chama cha TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION(TAA) kiliungana na chama cha  AFRICAN ASSOCIATION (AA) Kuunda chama kimoja kijulikanacha kama TANGANYIKA  AFRICAN NATIONAL UNION (TANU).
Waasisi wa Tanu wakiwa na baadhi ya vijana waliokuwa walinzi wao.(picha na Mohammed Said Blog)

Mara tu baada ya UHURU wa Tanganyika, serikali ilihimiza suala zima la kilimo ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza uchumi na kuleta ustawi mzuri kwa wananchi wa Tanzania. Jambo  hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani wananchi walipata elimu ya kutosha kuhusiana na kilimo, pia iliamuliwa kuwa kila kiongozi wa chama lazima awe na shamba la mfano ili wananchi waweze kujifunza kutoka kwao. Hapo ndipo ilipoanzishwa sera ya SIASA NI KILIMO.
Muonekano wa Sabasaba kwa hivi sasa

Hivyo, kila mwaka kukawa na maonesho ya sabasaba lengo likiwa ni kuonesha kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa TANU pia kukumbuka malengo ya msingi ya chama cha TANU ambapo ni pamoja na kuendeleza kilimo ambacho ni UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU. 

 
Nafasi hiyo ilitumika pia na wakufunzi pamoja na wanafunzi wa vyuo vya kilimo hususani chuo cha SUA (SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE) kuonesha ugunduzi wa mbegu mpya za kisasa, dawa bora za kuua wadudu au mbinu mpya ya kuongeza mazao ya kilimo. Kwa wakati huo serikali ilijali sana kazi za wakulima hata kutenga siku maalumu kwa ajili yao, ndio maana siku hizi karibu kila mkoa kuna eneo linaitwa sabasaba ambayo ni maeneo ya kibiasha.
Kitu cha kushangaza ikafika kipindi wakulima hao ambao ni siku yao ya kuonesha  mazao ya kazi za mikono yao wakawa wanatozwa pesa za kuingilia na kulipia eneo ambalo watakuwa wanafanya biashara zao, kitu ambacho ni tofauti kabisa na malengo ya siku hiyo ya sabasaba.
Baadhi ya mabanda ya wafanya Biashara katika

Kadiri miaka ilivyozidi kwenda, ndipo wakulima wakawa wanashindwa kuja kuonesha bidhaa zao kutokana na gharama kubwa zilizokuwa zikitozwa. Nafasi ya wakulima ikachukuliwa na wafanyabiashara ambao walikuwa wanaweza kulipia gharama zote ambazo walikuwa wakitozwa, na mpaka sasa adhma ya sabasaba kuwa ni siku ya WAKULIMA imegeuzwa na kua siku ya WAFANYABIASHARA tena wa viwandani.
Kutokana na unyonge wa wakulima wetu ikabidi wapewe siku nyingone ambayo ni siku ya nane nane ili waweze kuadhimisha siku ya kilimo rasmi badala ya siku ya sabasaba kama ilivyo hapo awali na mpaka sasa wakukima huadhimisha siku yao ya nanenane na wafanyabiashara huadhimisha siku ya sabasaba, kitu ambacho ni tofauti na malengo yaliyowekwa na TANU.
Lakini tukumbuke kuwa, wakulima wa nchi hii ndio wanoijenga serikali, kwa maana ya kwamba wao ni zaidi ya 75%  ya wananchi wote ndio wapiga kura, lakini hawathaminiwi kila siku bei za pembejeo za kilimo zinaongezeka.
Naomba tukubaliane ya kwamba siku ya sabasaba ni siku ya kuadhimisha kuanzishwa kwa TANU na sio vinginevyo.     


No comments:

Post a Comment